AJALI MBAYA YATOKEA IRINGA, WATU 38 WAJERUHI

Daladala 
aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake 
za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu 
Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha 
Bibi.


Taxi 
ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari
 polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika 
eneo la tukio.(P.T)

Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajari hiyo katika mlima wa Ipogolo (Kisima cha Bibi).

Basi aina 
ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo 
la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali 
iliyojeruhi zaidi ya watu 30.
ZAIDI ya 
abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini 
Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na 
kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana
 wa siku ya jana.
Tukio hilo limetokea katika mlima wa 
Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali 
hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa 
mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi 
breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari 
matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa,
 Tax pamoja na Hiace.
Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio
 hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. 
Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 
huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi 
wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi
 nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
MWISHO
Chanzo:Oliver Motto
No comments:
Post a Comment