TANZANIA KUTOA MSIMSMI WIKI HII KUTWENGWA NA EAC

Tanzania imesema itatoa msimamo wake 
wiki hii kuhusu mkutano wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika 
Mashariki (EAC) ngazi ya marais, uliotarajiwa kufanyika jana kujadili 
masuala yanayohusu maslahi ya nchi zilizoko katika ukanda huo bila 
kushirikishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika 
Mashariki, Samuel Sitta, aliliambia NIPASHE mjini hapa jana kuwa mkutano
 huo ulitarajiwa kufanyika nchini Rwanda jana na kwamba ungehusisha 
marais wa nchi za Rwanda, Paul Kagame; Rais wa Uganda, Yoweri Museveni; 
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
Alisema hayo alipokuwa akijibu swali 
la NIPASHE lililotaka kauli ya serikali kuhusu uamuzi wa nchi hizo 
kuendeleza tabia yao ya kuitenga Tanzania katika mikutano yao.(P.T)
            
"Mkutano wa Rwanda unafanyika leo 
ngazi ya marais. Tunasubiri kupata maazimio. Tanzania itatoa msimamo 
wiki hii," alisema Waziri Sitta bila kutaka kuingia kwa undani kuhusiana
 na suala hilo.
Mkutano huo ni wa tatu kufanyika bila kuishirikisha Tanzania. Mara mbili mfululizo, marais wa nchi hizo walikutana na kujadili mchakato wa kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo, huku wakiitenga Tanzania.
Marais Kenyata, Museveni na Kagame alikutana mara zote hizo bila kumualika Rais Jakaya Kikwete.Kwenye vikao viwili vilivyofanyika nchini Uganda na Kenya, viongozi hao walikubaliana kutekeleza kwa haraka miradi ya ujenzi wa reli itakayounganisha nchi hizo na bomba la mafuta litakalojengwa kuanzia Sudan Kusini hadi Mombasa na lingine kutoka Kenya hadi Rwanda.
Pia nchi hizo zilitangaza kuanzia Januari Mosi, raia wao watembeleane bila kuwa na hati za kusafiria, pia kuwa na viza moja kwa watalii.
Mkutano wa Kenya ulioambatana na ufunguzi wa gati katika bandari ya Mombasa, nchi za Burundi na Sudani Kusini zilialikwa na kuwakilishwa na mawaziri wao waandamizi, lakini Tanzania haikualikwa.
Vile vile, vyombo vya habari viliwakariri baadhi ya mawaziri wa nchi hizo waliopewa jukumu la kusimamia makubaliano hayo, wakiyaeleza kuwa ni ya jumuiya nzima na endapo Tanzania ikipenda kuingia itakaribishwa. Kutokana na hali hiyo, Serikali ya Tanzania ilionyesha wasiwasi wake juu ya mwenendo wa nchi hizo.
Ilipinga dalili zinazoonekana kwa nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kutumia jina la EAC kuomba fedha au kugharimia miradi inayopaswa kuwa ya jumuiya.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Abdullah Juma Saadalla.
Alisema malalamiko hayo yalishawasilishwa pia katika kikao cha Baraza la Mawaziri wa EAC, kilichofanyika jijini Arusha.
Dk. Saadalla alisema serikali imemtaka Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera, kutoa maelezo juu ya gharama ya miradi kadhaa inayoaminika kuwa sehemu ya jumuiya hiyo. Pia alisema hatua zilizochukuliwa na nchi hizo kwa kukubali kuanzisha utaratibu wa matumizi ya viza moja na vitambulisho vya pamoja, ni mfano wa ubabe usiokidhi matakwa ya kidemokrasia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema hivi karibuni kuwa Tanzania ikibaini kuwapo haja ya kujitoa EAC itafuata utaratibu kwa kulifikisha suala hilo bungeni ili wabunge waliamue.
CHANZO: NIPASHE
                    
No comments:
Post a Comment