TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, October 22, 2013

MARANDA ,WENZAKE KUJITETEA NOVEMBA 18

bot_b0655.jpg
Kada wa CCM, Rajabu Maranda, binamu yake Farijala Hussein na wafanyakazi watatu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Novemba 18, mwaka huu wanatarajiwa kuanza kutoa utetezi wao katika kesi inayowakabili.
Kesi hiyo inahusisha wizi wa Sh 207 milioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) iliyopo BoT.
Wakili wa Serikali, Awamu Mbangwa, jana aliliambia jopo la mahakimu watatu kuwa kesi hiyo, ilifikishwa kwa ajili ya washtakiwa kuanza kutoa ushahidi.
Jopo linalosikiliza kesi hiyo, linaoongozwa na Jaji John Utamwa, akisaidiwa na Jaji Ignas Kitusi na Jaji Eva Nkya.
Mawakili wa utetezi, Wabeya Kung'e na Rose Rutha, nao walisema kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya wateja wao kuanza kujitetea lakini mshtakiwa Rajabu Maranda hayupo na wakili wake Majura Magafu hivyo waliomba iahirishwe.(P.T)
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Jaji Utamwa alikubali na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 18, mwaka huu.
Washtakiwa Rajabu, Farijala na wafanyakazi wa BOT, Ester Komu, Bosco Kimera na Imani Mwakosya kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za uongo, kughushi na kuiba jumla ya Sh 207 milioni kutoka kwenye Akaunti ya EPA. Nyaraka hizo za kughushi ni pamoja na hati za makubaliano ya kuhamishiwa deni kutoka Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ambazo inadaiwa walizutumia na kuiba Sh 207,284,391.44.
Maranda na Farijala tayari wanatumikia vifungo vya nyakati mbalimbali jela, baada ya kupatikana na hatia katika kesi tatu zinazohusu wizi wa fedha za EPA.

No comments:

Post a Comment