WAKIMBIZI WA SYRIA WATESEKA MISRI

Shirika la kimataifa Amnesty 
International,linasema kuwa maafisa nchini Misri wanawazuilia mamia ya 
wakimbizi wa Syria katika mazingira mabaya sana.
Wakimbizi hao wanatoroka vita vinavyoendelea Syria.
Katika ripoti yake mpya, shirika hilo linasema kuwa idadi kubwa ya watoto wanazuiliwa wengi wakiwa hawana wazazi.
Kwa mujibu wa shirika hilo, baadhi ya 
wakimbizi wamezuiliwa katika vituo vya polisi ambako hali ni duni wengi 
wakiwa hawapati chakula wala matibabu kwa walio wagonjwa.
Linasema kuwa mjini Alexandria , mapacha wawili wenye mwaka mmoja walipatikana miongoni mwa wale waliozuiliwa.
Maafisa wa utawala bado hawajajibu tuhuma za shirika hilo.
Misri imekuwa ikikumbwa na vurugu za kisiasa tangu kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Hosni Mubarak mwaka 2011.(P.T)
No comments:
Post a Comment