JE WANAJESHI WA KENYA WALIPORA WESTAGE?
Picha za wanajeshi wa Kenya
waliokwenda katika jumba la Westgate katika juhudi za uokozi na kisha
baadaye kuonekena kwenye kamera za CCTV wakiondoka na mifuko ya
plasitiki yenye bidhaa za madukani, bila shaka zimewashangaza wengi.
Picha hizo mwanzo zimeonyesha
wanajeshi wakiingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamebeba silaha
kukabiliana na wanamgambo walioshambulia jengo hilo wiki nne zilizopita
na baadaye wakitoka wakiwa wamebeba mifuko hiyo wakiwa na silaha zao kwa
wakati mmoja.
Hata hivyo haijulikani walichokuwa wamekibeba kwenye mifuko hiyo .
Pamoja na picha za wanajeshi wakiwa
wamebeba mifuko, pia kulikuwa na picha zengine zilizoonyesha mashine ya
pesa zikiwa zimeporwa ndani ya mikahawa huku picha za alama za risasi
kwenye maeneo ya kuhifadhia pesa, pia zikionekana.(P.T)
Inaarifiwa ilikuwa jaribio ya kufungua hifadhi hizo ambalo halikufanikiwa.
Madai haya ya wanajeshi kufanya uporaji wa maduka katika jingo hilo, yalikanushwa vikali na jeshi la Kenya kiasi cha kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanatoa madai hayo, lakini haijulikani jibu lao litakuwa nini hasa kwa picha hizo za CCTV zilizoonyesha wanajeshi hao wakifanya uporaji.
Wamiliki wa maduka waliorejea kwenye maduka yao bbaada ya shambulizi , walidai kuwa maduka yao yaliporwa ingawa jeshi lilikanusha madai hayo baadhi ya taarifa zikisema kuwa ilikuwa njama ya wafanyabiashara kudai fidia kwa mali zao zilizoharibika.
Sio wanajeshi pekee waliotuhumiwa kwa uporaji, kwani polisi mmoja naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la uporaji baada ya kupatikana na pochi la mtu liliokuwa na damu.
Wangambao wa Al Shabaab waliteka nyara jengo la Westgate kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu 60 pamoja na kuwajeruhi zaidi ya watu miamoja.

No comments:
Post a Comment