Picha za ajali ya pili aliyoipata David Beckham na mwanae

Staa
 wa soka David Beckham (38) pamoja na mtoto wake wa kwanza aitwae 
Brooklyn walipata ajali ndogo nje ya nyumba yao huko Beverly Hills 
Marekani baada ya gari lao kugongana na gari jingine wakati wakitoka 
nyumbani.
Hakuna alieumia kwenye hii ajali ambayo iliihusisha Range Rover ya 
Beckham yenye thamani ya dola za Kimarekani elfu 75 ambapo iliumia 
sehemu ya mbele na mashuhuda wanasema baada tu ya ajali David Beckham 
hakuondoka kwenye eneo la tukio, alichofanya ni kusubiri Polisi.
Hii inakua ajali ya pili ya gari kwa Beckham kuipata akiwa na mtoto 
wake huyu wa kwanza mwenye umri wa miaka 14, kama unakumbuka ajali ya 
kwanza waliipata mwaka 2011 huko Los Angeles ambapo hakuna aliejeruhiwa.




No comments:
Post a Comment