KOMBE LA CHALENJI: SERIKALI YA KENYA YASEMA HAINA FEDHA ZA KUANDAA MICHUANO HIYO
Serikali ya Kenya imesema haina fedha
kwaajili ya kuandaa Michuano ya Chalenji ya mwaka huu ambayo imepangwa
kupigwa Novemba 27 hadi Desemba 12 Nairobi,Kenya.
Tamko hilo ni pigo zito waandaaaji wa
michuano hiyo ambao ni Baraza la Vyama vya Soka la Nchi za Afrika
Mashariki na Kati (Cecafa) lililo chini ya Rais Leodegar Tenga na Katibu
Mkuu wake Nicholas Musonye.
Awali, Mwenyekiti wa Shirikisho la
Soka Kenya(FKF), Sam Nyamweya alitangaza kuwa,michuano hiyo itaandaliwa
kwa ushirikiano wa pamoja kati ya shirikisho lake na Serikali ya nchi
hiyo.
Katibu wa Baraza la Michezo la
Kenya,Hassani Wario alisema, Serikali yake haitashiriki katika kuandaa
michuano hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti yake kwa sasa.(P.T)
"Kuandaa tukio kama hili kunahitaji fedha nyingi ambazo Serikali haina kwa wakati huu.
"Ni lazima tuwe wa kweli, hatuwezi kuungana na FKF na kudhamini mashindano hayo kwasababu hatuna bajeti kwaajili hiyo,"alisema Waria na kuongeza:
"Kuna vyama vingine ambavyo vinahitahi fedha kama ilivyo soka, kuogelea, wavu na hata Hockey, ni vigumu kujikita katika soka tu.
Hata hivyo, Musonye akizungumza na Mwananchi alisema:
"Tumeamua na ni lazima michuano hii ifanyike Kenya.
"Tunatafuta wadhamini wengine, lakini ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba mashindano yatafanyika hapa na hayawezi kuhamishiwa sehemu nyingine.
Mara ya mwisho Kenya iliandaa michuano ya Chalenji mwaka 2009 ambapo Uganda ilifanikiwa kutwaa ubingwa.
SOURCE: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment