TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, October 23, 2013

KABILA KUTANGAZA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA KARIBUNI 

kabila 21d7b
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema ataunda serikali ya umoja wa kitaifa hivi karibuni kufuatana na mapendekezo yaliyotolewa na mkutano wa kitaifa ulomalizika Oktoba 5 2013. (HM)

Katika hotuba nadra aliyotowa mbele ya mabaraza mawili ya bunge siku ya Jumatano kiongozi huyo alisema "serikali hiyo itakuwa na wajumbe wa mungano wa vyama tawala, upinzani na mashirika ya kiraia kwa lengo la kudumisha amani na utawala wa kitaifa kote nchini pamoja na kuimarisha umoja, kuikarabati nchi, na kukamilisha utaratibu wa madaraka mikowani.
Baadhi ya vyama vya upinzani vinapinga wazo hilo la serikali ya umoja wa kitaifa, vyama hivyo vinaeleza kwamba havijahusishwa kikamilifu katika mazungumzo ya kitaifa na serikali haiwezi kufanikiwa bila ya kiongozi hyo kukutana na viongozi wakuu wa upinzani.
Mbunge wa Uvira na kiongozi wa chama cha upinzani cha UNC Justin Bitakwira, Biwanahai, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba ili upatanishi na maridhiano yaweze kukamilika ni lazima kwa Bw. Kabila kuzungumza kwanza na Bw. Etienne Tshisekedi na Bw. Vitale Kamerhe, viongozi wawili aliyewashinda katika uchaguzi mkuu ulopita ulokuwa na utata.
Viongozi hao wawili walisuisia pia mazungumzo ya kitaifa yaliyoitishwa na Rais Kabila.
Akizungumzia suala la mazungumzo ya Kampala kati ya serikali na kundi la M23, Rais Kabila amesema, mazungumzo yamechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa na kwamba hapatakuwa na msamaha kwa waasi walotenda uhalifu wa kuchukiza na wapiganaji hawatoandikishwa katika jeshi la Taifa.
Mwakilishi wa Marekani kwa ajili ya Mataifa ya Maziwa Makuu Russ Feingold alisema mjini Kinshasa siku ya Jumatano kamba serikali ya Washington inaunga mkono msimamo wa Kinshasa na kwamba mazungumzo ya Kampala yanabidi kupelekea kuvunjwa kwa kundi la M23.
Hata hivyo msemaji wa M23 Amani Kabasha, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba kundi lake limeshtushwa na tangazo hilo la Kabila, na kutowa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kusaidia ili mazungumzo yaweze kumalizika na amani kupatikana huko Kongo. Chanzo: voaswahili

No comments:

Post a Comment