TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, October 19, 2013

JANUZAJ KUBAKI MAN U, ANATAKA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA 

man u d9d7f
KINDA Adnan Januzaj amesema kwamba anataka kuongeza Mkataba kuendelea kucheza Manchester United. (HM)

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18, alifunga mabao mawili dhidi ya Sunderland katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England kwa mabingwa hao watetezi na anatarajiwa kusaini Mkataba wa muda mrefu Old Trafford.
Mkataba wa sasa wa Januzaj unatarajiwa kumalizika Juni 2014 na vigogo wa Ulaya, Juventus na Barcelona wanataka saini ya kiungo huyo, lakini anatarajiwa kubaki United na kusaini Mkataba mpya.
"Nina furaha Manchester United na ninataka kujifunga kwa asilimia 100 kufanya vizuri katika kila mechi," Januzaj aliiambia Shirika Televisheni ya Kosovo, KTV.

"Nataka kuisaidia Manchester United kushinda ubinga wa Ligi Kuu na kuwa mchezaji bora duniani,".
Mustakabali wa soka ya kimataifa bado haueleweki kwa Januzaj, pamoja na hayo kinda huyo haruhusiwi kuichezea England hadi awe ameishi kwa miaka mitano nchini humo.
Amekwishaishi England kwa miaka miwili, hivyo atalazimika kusubiri hadi mwaka 2016.
"Ni baba yangu anayemua nichezee timu gani ya taifa, nitachezea atakapoamua, hivyo nitamsikiliza yeye,"alisema Januzaj. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment