JK ATEMBELEA NA KUKAGUA JENGO LA BUNGE MJINI DODOMA lEO

Rais wa 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, 
Alhamisi, Oktoba 24, 2013 ametembelea na kukagua Jengo la Bunge la 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kujionea maandalizi ya 
jinsi Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba watakavyokaa katika Ukumbi wa 
Bunge hilo. Bunge hilo Maalum la Katiba litakuwa na Wabunge 600 tofauti 
ya Bunge la sasa lenye Wabunge 354 ambao ni pamoja na Wabunge 239 wa 
kuchaguliwa kutoka majimboni, Wabunge Wanawake Viti Maalumu 102, Wabunge
 wa kuteuliwa toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar 5, Mwanasheria Mkuu wa
 Serikali na Wabunge 7 (kati ya 10) wa kuteuliwa na Rais. (HD)

No comments:
Post a Comment