MAGARI MAALUMU TU MECHI YA SIMBA, YANGA
Magari
yenye shughuli maalumu tu ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanja wakati
wa mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa keshoku(Jumapili) kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi itaanza saa 10 kamili jioni, na kila timu inaruhusiwa kuingia
na magari matatu tu; gari la timu na mengine mawili ya viongozi. Ukaguzi
wa kuingia uwanjani ni kwa watu wote, kwani utaratibu huo si wa
kumdhalilisha mtu bali lengo lake ni kuhakikisha usalama.
Vilevile watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na mifuko ya aina
yoyote ikiwemo mabegi, isipokuwa kwa waandishi wa habari wanaotumia
mabegi hayo kwa ajili ya kubebea kamera zao. Pia hakuna wafanyabishara
watakaoruhusiwa kufanya biashara katika maeneo yanayozunguka uwanja.
Kwa washabiki watakaokuwa katika mazingira ya kuwa kero kwa wenzao
wakiwemo walevi hawataruhusiwa kuingia uwanjani, pamoja na wale wenye
silaha kama bastola ambapo wakikamatwa wafikishwa polisi na baadaye
kufunguliwa mashtaka kortini.
Barabara ya Uwanja wa Taifa itafungwa kuanzia saa 2 asubuhi upande wa
Chang’ombe, hivyo washabiki wanatakiwa kununua tiketi zao mapema leo
(Jumamosi) ambapo zitaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali kuanzia saa 4
asubuhi.
Vituo hivyo ni mgahawa wa City Sports Lounge, Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa
Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala,
Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama na BMM Salon
iliyoko Sinza Madukani.
No comments:
Post a Comment