ENGLAND YAIFUMUA MONTENEGRO 4-1

Wayne Rooney akiifungia England bao la kwanza (HM)

ENGLAND imeongeza matumaini ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kuifumua Montenegro mabao 4-1 usiku huu.
Mabao ya England inayofundishwa na Roy
Hodgson yamefungwa na Rooney dakika ya 48, Boskovic akajifunga dakika
ya 62, Townsend dakika ya 78 na Sturridge dakika ya 90 kwa penalti,
lakini la wageni limefungwa na Damjanovic dakika ya 71.
Kikosi cha England kilikuwa: Hart,
Walker, Cahill, Jagielka, Baines, Gerrard/Milner dk87, Lampard/Carrick
dk65, Townsend/Wilshere dk80, Rooney, Welbeck na Sturridge
Montenegro: Poleksic,
Pavicevic/Beciraj dk57, Kecojevic, Savic, Jovanovic, Zverotic, Drincic,
Boskovic, Volkov/Vukcevic dk72, Damjanovic na Jovetic/Kazalica dk81.
Nayo Ujerumani imeendeleza ubabe baada
ya kuifumua Jamhuri ya Ireland mabao 3-0 usiku huu, shukrani kwao
Khedira aliyefunga dakika ya 12, Schurrle dakika ya 58 na Ozil dakika ya
90. Chanzo: sportmail
No comments:
Post a Comment