TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, October 18, 2013

WATOTO WAUAWA KWA BOMU SUDAN KUSINI 

110923041753_south_sudan_map_304x171_1_nocredit_c3750.jpg
Watoto watano wameuawa kwa bomu wakati walipokuwa wakichimba chuma chakavu katika eneo la mji mkuu wa Juba, Sudan Kusini.
Watoto hao walikuwa wakitafuta vyuma hivyo katika eneo la makazi ya zamani wanajeshi, msemaji wa Jeshi ameiambia BBC.
Mwandishi wa Habari wa BBC James Copnall amesema baruti ambazo hazijalipuka kwenye migodi bado ni tatizo kubwa Sudan Kusini kufuatia miongo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kuna operesheni maalum ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Sudan Kusini, lakini milipuko imekuwa ikiua watu kila mwaka.(P.T)
Watoto wenye umri kati ya miaka 10 na 14 wameuawa katika eneo la makazi ya wanajeshi ya zamani katika wilaya ya Souk Sita katika mji wa Juba, msemaji wa Jeshi Kanali Philip Aguer amesema.
Amesema raia wa Uganda aliyekuwa pamoja watoto hao akitarajia kununua vyuma hivyo chakavu naye amejeruhiwa.
Sudan Kusini ilipata uhuru mwaka 2011 baada ya muda mrefu wa migogoro na Sudan na kubakia miongoni mwa mataifa maskini sana duniani.

No comments:

Post a Comment