TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, October 30, 2013

MIILI 87 YA WAHAMIAJI YAPATIKANA JANGWANI

 miili_71e3a.jpg

Waokozi nchini Niger wanasema kuwa wamepata miili 87 ya watu waliofariki baada ya magari yao kuharibika walipokuwa wanajaribu kuvuka jangwa la Sahara.
Mmoja wa waliokuwa wanaendesha shughuli ya ukozi Almoustapha Alhacen, alisema kuwa miili yao ilikuwa katika hali mbaya ya kuharibika na kuwa ilikuwa imeliwa sehemu moja na wanyama pori.
Miili hiyo inaaminika kuwa ya wafanyakazi wahamiaji na familia zao. Wengi walikuwa wanawake na watoto.
Niger ni kivukio kikubwa cha wahamiaji wanaokuwa safarini kufika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuelekea Ulaya.
Lakini wengi wa wanaofanikiwa kukamilisha safari hiyo huishia kufanya kazi katika mataifa ya Afrika Kaskazini.(P.T)
Kulingana na Bwana Alhacen, moja ya magari ambayo wahamiaji hao walikuwa wanatumia kwa usafiri, liliharibika walipotoka mji wa Arlit mwishoni mwa mwezi Septemba, au mwanzoni mwa Oktoba.
Maafisa wa usalama pia wamesema kuwa gari la pili liliharibika lilipokuwa njiani kurejea Arlit ili kutengenezwa.
Inaonekana kuwa miongomi mwa wasafiri hao takriban watu 10 walisafari kurejea Arlit na kutoa taarifa ya wenzao kukwama jangwani.
Iliarifiwa kuwa miili mitano ilipatikana.
Mnamo siku ya Jumatano, wafanyakazi wa kujitolea pamoja na wanajeshi, walipokuwa wanawatafuta wahamiaji hao, wakafanikiwa kupata maiti zaidi umbali wa kilomita 10 kutoka katika mpaka wa Algeria.
Kati ya maiti 48 waliopatikana, kulikuwa na miiili ya watoto na vijana na Alhacen alisema kuwa walikuwa wanaelekea nchini Algeria kutafuta vibarua vya mishahara midogo sana.
Akizungumza kutoka katika kiwanda cha kuchimba madini ya Uranium, Kaskazini mwa Agadez, aliambia BBC kuwa hiyo ndiyo iliuwa siku mbaya kwake baada maishani mwake baada ya kupata miili hiyo.

No comments:

Post a Comment