DEFOE AING'ARISHA SPURS ikiishinda FC Sheriff 2-0
MSHAMBULIAJI Jermain Defoe kwa mara
nyingine amedhihirisha hajachuja baada ya kuifungia bao Tottenham katika
ushindi wa 2-0 dhidi ya FC Sheriff Tiraspol kwenye Europa League na
kuvunja rekodi ya mabao ya Martin Chivers iliyodumu kwa miaka 40 katika
michuano ya Ulaya. (HM)
Shujaa wa miaka ya sabini, Big Chiv, mshindi wa Kombe la UEFA akiwa na Spurs mwaka 1972, alisema amefurahi kufikiwa idadi yake ya mabao, 22 na mshambuliaji tegemeo la Spurs hivi sasa.
Defoe, alianza katika nafasi ya Roberto Soldado, akiwa amefunga mabao sita katika msimu huu wa Europa League na usiku huu akafunga tena dakika ya 75 baada ya Vertonghen kutangulia Spurs dakika ya 12 katika ushindi wa 2-0
Kikosi cha Tottenham kilikuwa: Lloris, Naughton, Chiriches, Vertonghen, Fryers/Dawson dk34, Dembele, Sandro/Holtby dk76, Lamela/Chadli dk61, Eriksen, Lennon na Defoe.
Sheriff: Tomic, Balima, Paye, Moyal/Furdui dk70) Samardzic, Metoua, Cavalcante Mendes, Stanojevic, Isa Mustafa/Paireli dk88, de Fiori Mendes/Gomes de Jesus dk84 na Henrique de Sousa.
No comments:
Post a Comment