WANAFUNZI WAPAMBANA NA POLISI CAIRO
Polisi wa Misri wamefyatua moshi wa
kutoza machozi kuvunja maandamano mjini Cairo, ya wanafunzi wanaomuunga
mkono rais wa zamani, Mohamed Morsi.
Mawe yalirushwa na pande zote mbili
huku wanafunzi mia kadha wakijaribu kutoka chuoni kuelekea Medani ya
Rabaa, pahala pa kambi ya wafuasi wa Morsi ambayo ilifungwa na wakuu
miezi miwili iliyopita.
Hii ni siku ya pili ya mapambano
katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambako kuna wafuasi wengi wa chama cha
Muslim Brotherhood cha Bwana Morsi.
Bwana Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwezi wa Julai.(P.T)
No comments:
Post a Comment