Alichosema David Beckham kuhusu kumkosoa Sir Alex Ferguson juu ya ile kauli
Tunafahamu
 kwamba siku Sir Alex Ferguson anazindua kitabu chake ambacho ameandika 
mambo mbalimbali kuhusu kazi yake kwa miaka yote akiifundisha club ya 
Manchester United, aliweka wazi kwamba alimuuza Beckham kwenda Real 
Madrid 2003 kwa sababu staa huyu wa soka alijiona yeye ni mkubwa kuliko 
Manager, alijiona mkubwa kuliko club na kwamba alipoanza mapenzi na 
Victoria ndio kama alianza kulegeza uzi kwenye kazi.Pamoja na hayo maneno ambayo ndio yalipewa headlines za kutosha huku wengi wakiamini kwamba yatamkasirisha Beckham, staa huyu ameileta hii ishu kwenye upande mwingine baada ya kusema hawezi kumponda Sir Ferguson wala kusema chochote kibaya kuhusu Mwanaume huyu aliesababisha ndoto zake za kuwa staa wa soka kutimia.

Beckham ambae amepongezwa na wengi kwa hekima hii, anakwambia ‘Sir Ferguson ndio aliniamini na kunipa nafasi, siwezi kukaa hapa kuongea mabaya au kumkosoa mtu alienifanya niishi kwenye ndoto yangu niliyoitaka toka kitambo’
No comments:
Post a Comment