MSUMBIJI U 20 KUWASILI OKTOBA 25

Timu ya 
Taifa ya wanawake kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 inawasili 
nchini kesho (Ijumaa, Oktoba 25 mwaka huu) saa 8.30 mchana tayari kwa 
mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania 
itakayofanyika Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu). (HD)
Msumbiji 
itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege 
ya LAM ikiwa na msafara wa watu 25 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi 
na viongozi. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Sapphire iliyopo maeneo
 ya Gerezani, Dar es Salaam.
Mara 
baada ya kuwasili JNIA, kocha na nahodha wa timu hiyo watazungumza na 
waandishi wa habari juu ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar
 es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Kwa 
upande wa U20 chini ya Kocha Rogasian Kaijage imejiandaa vizuri kwa 
ajili ya mechi hiyo, na kesho saa 10 jioni itafanya mazoezi yake ya 
mwisho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio
 kwa mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na rangi
 ya chungwa. Viingilio vingine ni sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP
 B wakati VIP A itakuwa sh. 10,000.
Kamishna 
wa mechi hiyo Evelyn Awuor kutoka Kenya tayari amewasili nchini wakati 
waamuzi kutoka Burundi wanatarajia kuwasili leo saa 1 usiku kwa ndege ya
 Kenya Airways wakiunganishia safari yao Nairobi, Kenya. Maofisa wote wa
 mechi hiyo wanafikia hoteli ya New Africa.
UCHAGUZI TPL BOARD KUFANYIKA IJUMAA
Uchaguzi 
wa Bodi ya Ligi Tanzania (Tanzania Professional League- TPL Board) 
unafanyika kesho (Oktoba 25 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano uliopo 
Golden Jubilee Tower kuanzia saa 3 asubuhi.
Mgeni 
rasmi katika mkutano huo wa Bodi ya TPL ambao unafanyika kwa mara ya 
kwanza atakuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), 
Leodegar Tenga.
Kwa 
mujibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, wajumbe wanaounda Mkutano wa 
Uchaguzi ni wenyeviti kutoka klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na
 14 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Viongozi 
wa klabu za FDL wamefikia hoteli ya Royal Valentino iliyoko Barabara ya 
Uhuru wakati wale wa VPL ambao pia watashiriki Mkutano Mkuu wa 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamefikia hoteli ya Landmark
 iliyopo Ubungo.
Wagombea 
kwenye uchaguzi huo ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Said Muhammad Said
 Abeid (Makamu Mwenyekiti) wakati wanaoomba ujumbe wa Kamati ya 
Uendeshaji ni Khatib Omari Mwindadi na Kazimoto Muzo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment