
FREEMAN MBOWE.
Hatua
hiyo inatokana na msimamo wa wabunge wa vyama hivyo kususia mjadala wa
muswada huo uliopitishwa hivi karibuni na wabunge wachache wa CCM na
Augustine Mrema wa TLP, wakidai umechakachuliwa, huku Zanzibar ikiwa
haijashirikishwa.

PROF IBRAHIM LIPUMBA.
Kufuatia
kusigana huko, viongozi wa vyama hivyo; Freeman Mbowe (CHADEMA), Prof.
Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi), walikutana na
makundi mbalimbali ya wadau na kutangaza kufanya mikutano na maandamano
nchi nzima kupinga rais asisaini muswada huo.

JAMES MBATIA.
Uamuzi
wa wapinzani hao uliwaibua mawaziri kadhaa, Stephen Wassira (Ofisi ya
Rais-Mahusiano na Uratibu), William Lukuvi (Sera, Uratibu na Bunge),
Mathias Chikawe (Katiba na Sheria) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji
Frederick Werema wakiwabeza.
Mawaziri
hao walidai wapinzani wanapoteza muda wa mchakato ili rais awaite Ikulu
tena kwa mazungumzo waweze kunywa chai na juisi, jambo walilosisitiza
kuwa haliwezekani, kwani milango hiyo imefungwa.
Hata
Waziri Chikawe alifikia hatua ya kumtisha Rais Kikwete, akisema kuwa
asipousaini muswada huo atakuwa ametangaza mgogoro na Bunge, kwani
lilifanya kazi yake kwa kufuata Katiba.
Rais
Kikwete alitilia maanani hoja za pande zote na kuamua kuwaita wapinzani
mezani kuzungumza nao, akisema kuwa kama dhamira yao ni kutaka kupata
Katiba mpya, anawashauri waachane na mipango ya maandamano na kufanya
ghasia, bali watumie njia halali, kwamba serikali iko tayari
kuwasikiliza.
Hoja zinazovutaniwa
Mbali
na mambo mengine, wapinzani wanadai kuwa muswada huo ulichomekwa baadhi
ya vipengele ambavyo vingeisaidia CCM kutawala mchakato mzima wa
katiba.
Katika
hoja ya mapendekezo ya kumpa rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge
Maalumu, wapinzani hao wanasema hayakubaliki, kwamba yanarudisha dhana
kwamba wajumbe hawa watakuwa watu wa rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa
CCM.
“Sheria
iweke wazi kwamba wajumbe hawa ‘watateuliwa’ na taasisi zilizotajwa.
Hii itaondoa utata juu ya uwakilishi wao na juu ya mamlaka yao ya
uteuzi.
“Sheria
itaje kwamba idadi ya wajumbe wa Bunge Maalumu watakaotokana na kila
taasisi iliyoorodheshwa katika kifungu cha 22(1)(c) itakuwa 354,”
walisema wapinzani.
Katika
suala la Zanzibar, wapinzani hao wanasema wananchi wa huko
hawakushirikishwa wakati wa uandaaji wa muswada huo, hivyo kutaka mambo
kadhaa yafanyike ili kuondoa mgongano.
Kwamba,
ili kutimiza matakwa haya ya sheria na kwa kuzingatia mapendekezo ya
Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume, Bunge linahitaji kuangalia upya
suala la uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalumu.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 22(2) cha Sheria, idadi ya wajumbe wa Zanzibar
katika Bunge Maalumu watakaotokana na makundi yaliyoainishwa katika
kifungu cha 22(1)(c) “... haitapungua theluthi moja ya wajumbe hao.”
Hii ina maana kwamba, kwa uchache kabisa, wajumbe hao wa Zanzibar hawatapungua 55.
Rasimu
ya Katiba itakayojadiliwa na Bunge Maalumu inahusu Katiba ya Jamhuri ya
Muungano peke yake. Rasimu hiyo imependekeza kwamba masuala yote yasiyo
ya Muungano, ya washirika wa Muungano, yaani Tanzania Bara na Zanzibar,
yashughulikiwe na Katiba za washirika hao.
Rais
Kikwete katika kutambua hoja za wapinzani aliomba hekima ziwaongoze
viongozi wa pande zote ili waweze kutumia utaratibu walioutumia mwaka
2012.
“Kulipotokea
mazingira kama haya pande zote zilikaa pamoja na kuzungumzia hoja moja
baada ya nyingine na kukubaliana nini kifanyike na kifanyike vipi. Baada
ya kuridhiana hatua zipasazo za kisheria na kanuni zilichukuliwa na
kumaliza mzozo,” alisema rais.
Aliongeza
kuwa kufanya kinyume cha hayo hakutaleta ufumbuzi wa mzozo huu na
kutaliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima.
Rais
Kikwete alisisitiza kuwa hawatengenezi katiba ya chama fulani bali
katiba ya nchi, katiba ya watu wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama
ambao ndio wengi kuliko wote.
Kuhusu
ushiriki wa Zanzibar, alisema kuwa alielezwa ni kwa kiasi gani Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar ilivyoshirikishwa na kutoa maoni yake
yaliyojumuishwa katika muswada.
“Kama
ni hivyo, nashauri kuwa suala hili lirudishwe bungeni ili wabunge
walizungumze na kulifanyia uamuzi muafaka. Vinginevyo watu wataendelea
kulaumiana isivyostahili,” alisema.
Suala
la Tume ya Mabadiliko ya Katiba nalo litakuwa sehemu ya mjadala huo,
licha ya Rais Kikwete naye kuona umuhimu wake akitaka ihusike kwenye
hatua ya Bunge Maalumu.
“Nimeulizia
ilikuwaje? Nimeelezwa kuwa jambo hili halitokani na mapendekezo ya
serikali wala ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.
Limetokana na pendekezo la mbunge katika Bunge wakati wa kupitia vifungu
na kuungwa mkono na wabunge wengi.
“Nami
naiona hoja ya wajumbe wa tume kuwa na wajibu wakati wa Bunge Maalumu,
hasa wa kusaidia kufafanua mapendekezo ya tume,” alisema. TANZANIA
DAIMA.
No comments:
Post a Comment