Mahojiano na wadau wa darasa la Kiswahili Washington DC

Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi kusini mwa jangwa la sahara.
Kama tunavyojua, ni lugha ya taifa kwa
nchi za Tanzania naKenya, na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na visiwa vya Comoro.
Mtangazaji wa Jamii Production Mubelwa
Bandio akiwa na Wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya
ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly
pamoja na walimu Asha Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza(P.T)
Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa
kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika
iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Na inaaminika kuwa
lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani
Na matumizi yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.
Kiswahili sasa kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani, lakini pia inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia.
Kiswahili ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata jumuiya ya waTanzania hapa Washington DC wakaona ni jambo la busara kuanzisha darasa la kufunza Kiswahili kwa watoto hapa DMV.
Wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza wamekuwa wakarimu sana kujiunga nami katika studio za JAMII PRODUCTION hapa Washington DC.
KARIBU UUNGANE NASI

No comments:
Post a Comment