BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA OFISI ZA WAKALA YA SERIKALI MTANDAO ;
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili katika ofisi za
Wakala ya Serikali Mtandao zilizopo jengo la TTCL mtaa wa Samora leo
jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia shughuli za usimamizi wa
mifumo na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
katika uendeshaji wa shughuli za serikali.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na viongozi wa Wakala ya
Serikali Mtandao na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara
baada ya kupokea taarifa kuhusu maendeleo ya Tovuti Kuu mpya ya serikali
inayosimamiwa na Wakala ya Serikali Mtandao chini ya Ofisi ya Rais
Menejiment ya Utumishi wa Umma. Balozi Sefue amefafanua kuwa Tovuti Kuu
ya Serikali iliyoanzishwa itawawezesha wananchi kupata taarifa na huduma
mbalimbali zinazotolewa na serikali.(P.T)
Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akiongea na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa serikali
katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano katika shughuli za serikali kupitia Tovuti Kuu mpya ya
serikali iliyoanzishwa kwa lengo la kuboresha na kurahisisha utoaji wa
taarifa na huduma kwa umma, kuhamasisha ushirikishwaji wa raia katika
utoaji wa maamuzi yanayowahusu na kuwezesha uwepo wa serikali iliyo
wazi.
Baadhi ya
viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao iliyo chini ya Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na waandishi wa habari wakiwa katika
mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Picha na 5. Mwonekano mpya wa Tovuti Kuu ya Serikali ambayo inapatikana katika anuani ya www.egov.go.tz.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
No comments:
Post a Comment