SERIKALI YASEMA TEHAMA KUFIKA HADI VIJIJINI
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
SERIKALI imesema kwamba inatarajia
kuboresha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kila
kijiji ili huduma zake ziweze kuwa karibu na wananchi, hatua hiyo
itasaidia kuwapunguzia gharama wanazozitumia.
Aidha Serikali imeeleza kwamba
iteendelea kujenga uwezo wa kiufundi wa kuweza kuzuia uvujaji wa siri,
uhalifu na udhibiti wa sheria ndani ya vyombo vyake ili taarifa za siri
zisiweze kuvuja.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea ofisi ya Wakala
ya Serikali Mtandao(e GA) jijini Dares Salaam kwa ajili ya kuzungumza na
menejimenti na wafanyakazi.(P.T)
"Leo nimetembelea ofisi hii. Ni eneo
la kipaumbele kwa Serikali kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA kwa Serikali,
tija, kasi ya utendaji kazi na huduma za Serikali. Hivyo sehemu hii ni
muhimu ya kuifanya Serikali iwe karibu na wananchi. Tovuti hii iwe ni
dirisha la mwananchi kutatuliwa shida yake.,"alisema huku akitoa wito
kwa wananchi wawe tayari kuitumia.
Balozi Sefue alisema tatizo la
changamoto la TEHAMA kuhusu uvujaji wa siri lipo dunia nzima hata
Marekani wanakabiliana nalo ,hivyo ufumbuzi wake si kuachana nalo bali
kuzuia uvujaji huo na uhalifu kwa kujenga uwezo wa udhibiti.
"Lazima kuwe na udhibiti mfano wa
kisheria tayari tunayo sheria tutaendelea kuiboresha kulingana na
changamaoto zitakazo kuja," alisisitiza Balozi Sefue.
Alisema kupitia TEHAMA wananchi
wataweza kupata matibabu au elimu na kulizia huduma wanazotakiwa kuzipta
mfano miradi ya visima vya maji imefikia hatua zipi.
Aliongeza kuwa hivi sasa wakala huo
unaandaa mifumo ya kuwezesha Wizara, Idara na taasisi mbalimbali za
Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano.
Akizungumzia kuhusu ufikishaji wa
huduma katika maeneo ya vijijini, Mtendaji Mkuu wa (eGA) Dk. Jabiri
Bakari alisema watatumia ubunifu ili kuhakikisha huduma ya TEHAMA
inatumika kwenye maeneo hayo mfano kwa kutumia sehemu za mkononi za
kawaida.
Wakala hiyo ulianzishwa Julai mwaka
2012, ambapo taarifa mbalimbali za Serikali kutoka Wizara, Idara ,
wakala na taasisi zake zitapatikana kupitia mtandao wa wakala hiyo.
No comments:
Post a Comment