TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, June 2, 2014

Taarifa rasmi ya Yanga kuhusu uwenyekiti wa Manji na kocha Maximo

1908319_739353366128611_8170079415409113241_n 
Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay  Dar es salaam huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Yusuf Manji amewaongoza wanachama hai 1,560 kupitisha kipengele hicho kipya kwa ajili ya maslahi na faida ya anga kwani bila kufanya hivyo timu isingeweza kuruhusiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Aidha katika mkutano huo Manji amewatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa usajili unaendelea kufanyika na nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi utakapokamilika basi wataweka wazi kila kitu.
Kuhusu nafasi ya Kocha Mkuu Manji amesema Kamati ya Mashindano imemkabidhi mapendekezo yao na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Marcio Maximo aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ili kuja kukinoa kikosi cha Jangwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mama Fatma Karume aliongoza kikao cha wanachama kilichomuomba Manji kuendelea na uongozi ambapo mwenyekiti alitoka nje na kamati yake ya utendaji na waliporejea walikubali ombi hilo na kusema watafuata taratibu za kikatiba.
Mwisho kupitia mkutano mkuu wa leo wa wanachama,  wameazimia kuwaongezea muda wa mwaka mmoja Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja na Makamu wake Clement Sanga ili waweze kukamilisha masuala ya katiba na kuweza kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya katiba kupitishwa na TFF

No comments:

Post a Comment