FASTJET YAINGIA ZIMBABWE
KAMPUNI
ya ndege ya Fastjet imezidi kupanua huduma zake kwa kuongeza masafa yake
kwenda nchini Zimbabwe mara mbili kwa wiki ikitokea Dar es Salaam na
kufikia njia ya tatu ya kimataifa baada ya zile za Zambia na Afrika
Kusini.
Akizungumzia
uzinduzi huo, Mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo, Ed Winter, alisema
wamefikia hapo baada ya kupiga hatua kimafanikio katika maeneo ya huduma
zake kwenye maeneo ya awali.
"Pamoja
na huduma zetu kufanikiwa, katika maeneo yetu ya huduma hapo awali, bado
tunatambua mahitaji muhimu ya Watanzania na wananchi wa nchi jirani
kiuchumi, kwamba wanahitaji kufika kwa wakati katika masoko yao ya
kibiashara," alisema.
Waziri wa
Uchukuzi na Usafirishaji wa Zimbabwe, Dk. Orbet Mpofu, alisema nchi
yake imepokea kwa furaha taarifa za Fastjet kuichagua Zimbabwe kuwa
sehemu yake muhimu ya kutolea huduma zake, na kwamba itakuwa faraja na
mafanikio makubwa ya kibiashara.
"Itakuwa
hatua moja nzuri sana ya kiuchumi baina ya wafanyabiashara wa Zimbabwe
na Tanzania, kwa hiyo sisi tunawakaribisha sana Fastjet kwani tumekuwa
tukisikia sifa nzuri kuhusu huduma nzuri na bei nafuu mnazotoa," alisema
Dk. Mpofu.
Alisema
kuwa Zimbabwe inalenga kufanya mazungumzo ya kina na Fastjet ili kuona
kama itawekeza nchini humo katika nyanja ya usafirishaji na uchukuzi.
CHANZO TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment