Divock Origi Najivuania kuwa mkenya

Origi Ni bao la kujivunia kwa kenya familia yangu na Ubeljiji.
Na Mathias Canal
Mshambuliaji
 wa Lille ya Ufaransa , Mkenya Divorc Origi ambaye ni raiya ya Ubelgiji 
aliyeifungia Ubeljiji bao la pekee na la ushindi dhidi ya Urusi katika 
mechi yao ya pili ya kundi H amesema kuwa anajivunia kuwa mkenya licha 
ya kuwa anaiwakilisha Ubeljiji.
Bao hilo la dakika za mejeruhi za mechi hiyo ndiyo iliyoiwezesha Ubeljiji kufuzu kwa mkondo wa pili wa timu kumi na sita bora.
Origi 
ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba baada ya kuondoka kwa Romelu 
Lukaku alifuma bao hilo la kipekee kunako dakika ya 88 ya kipindi cha 
pili ya mechi hiyo alipopokea pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard .

Origi,
 mwanawe Mike Okoth, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, 
Harambee Stars atakua mchezaji wa kwanza wa Afrika Mashariki 
kuiwakilisha Ubeljiji, na yuko pamoja na wachezaji nyota kama vile 
Vincent Kompany wa Manchester City na Eden Hazard wa Chelsea.
Akizungumza
 na BBC Origi anasema:''aliamua kuichezea Ubeljiji baada ya kutilia 
maanani mambo mengi kama vile usimamizi mzuri wa kandanda nchini humo, 
mizizi yake ya kandanda iliyoko huko, marafiki, ushauri wa babake pamoja
 na Ubelgiji kufuzu kwa kombe la dunia kwani haijulikani ni mwaka upi 
Kenya itafuzu kwa kombe la dunia.
Origi aliiambia BBC kuwa anafurahia mizizi yake na kuwa anajivunia bao hilo na familia yake iliyokuwa uwanjani kumshabikia .
Origi alisema kuwa hii ilikuwa ni tukuio spesheli kwake kwa Kenya na Ubeljiji.
No comments:
Post a Comment