TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, June 13, 2014

DRC na Rwanda zapigana

Mapigano yameendelea kwa siku ya pili kati ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na wale kutoka Rwanda kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Milio ya risasi iliyodumu karibu saa mbili iliripotiwa kusikika mapema Alhamisi.
Pande hizo zimekuwa zikishutumiana kwa kuanza mapigano.
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inasema kuwa vikosi vya Rwanda viliingia Mashariki mwa Congo, kumteka nyara na kumuua mwanajeshi wake, huku nayo Rwanda ikisema kuwa wanajeshi wa Congo ndio walioingia nchini mwao na kuwafyatulia risasi.
Makabiliano yalianza Jumatano katika kijiji cha Kanyesheza, kilomita 20 kutoka Goma mji mkuu wa mkoa huo na kudumu kwa saa kadhaa.
Wanajeshi hao walishambuliana kwa zana nzito za kivita, asubuhi na mapema kwa mujibu wa mmoja wa walioshuhudia makabiliano hayo.(P.T)
Pande hizo mbili zimekuwa zikilaumiana huku afisa mmoja wa Rwanda akidai kuwa wanajeshi wa DRC ndio waliowashambulia kwanza.
Hata hivyo duru zinasema kuwa hapakuwa na majeruhi ingawa wanajeshi walikuwa wanafyuatuliana risasi kiholela.
Makabiliano hayo yamezuka baada ya pande hizo mbili kushambuliana Jumatano.
Nchi hizo mbili zimekuwa zikizozana na kulaumiana kwa uchochezi, hasa Rwanda ikidaiwa kuunga mkono harakati za waasi wa M23 nchini DRC. Waasi hao walikuwa wanadhibiti eneo la Mashariki mwa nchi kabla ya kutimuliwa na wanajeshi wa Uganda.
Mwaka jana Rwanda ilituhumu jeshi la DRC kwa kurusha makombora ndani ya nchi hiyo na hivyo ikaamua kujibu mashambulizi hayo kwa kuweka wanajeshi wake mpakani.
Rwanda mara kwa mara imekuwa ikishutumiwa kwa kuanza mizozo mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo madai inayoyakanusha.

No comments:

Post a Comment