TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, June 9, 2014

Mchekeshaji Tracy Morgan katika hali mbaya baada ya ajali

tracy 
Mchekeshaji maarufu wa nchini Marekani Tracy Morgan bado yupo katika hali mbaya kiafya kutokana na ajali mbaya ya gari aliyopata mwishoni mwa wiki.
Muigizaji huyo wa vichekesho anakabiliwa na majeraha ya kuvunjika mbavu, pua na mguu baada ya gari aliyokuwa akisafiria kugongwa na gari kubwa na kusababisha ajali mbaya.
tracy2
Baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake, Morgan ameanza kuonyesha matumaini lakini ataendelea kubaki hospitalini kwa wiki kadhaa akipatiwa matibabu, kwa mujibu wa msemaji wake.
Katika ajali hiyo iliyotokea mjini New Jersey muigizaji mwingine wa vichekesho Jimmy Mack, alipoteza maisha.

No comments:

Post a Comment