TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, June 9, 2014

Sababu kwanini Jeniffer Lopez hatopafomu kwenye ufunguzi wa kombe la dunia

jennifer-lopez-pitbull-claudia-leitteMichuano ya kombe la dunia inatarajiwa kuanza siku ya alhamisi wiki hii nchini Brazil kwa ufunguzi wa mechi kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia, lakini kama ilivyo kawaida kabla ya mechi husika ya ufunguzi kunakuwepo na sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo mikubwa. Mwaka huu wasanii Jennifer Lopez,  Claudia Leitte na Pitbull walipangwa kutumbuiza.
Lakini kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba JLO amegoma kwenda kutumbuiza kwenye sherehe hizo za ufunguzi pamoja na kwamba ndio msanii alioimba wimbo rasmi wa michuano hiyo. 
Staa huyo ambaye wiki iliyopita ameachana na mpenzi wake Casper Smart – leo hii jina lake halikuwemo kwenye listi ya wasanii watakaosindikiza sherehe za ufunguzi alhamisi hii.
Kwa mujibu wa FIFA,  Jennifer Lopez hatotumbuiza kwenyey sherehe hizo kutokana na ‘sababu za kiufundi’ ambazo hazikufafanuliwa ni zipi.
Hata hivyo wasanii wengine walioshirikiana na JLO kuimba wimbo wa ‘Ole Ole’ – Pitbull na Claudia Leitte watapafomu kwnye sherehe hizo.

 

No comments:

Post a Comment