MAUAJI MENGINE KENYA 20 WAUAWA WAJIR
Moja ya mashambulizi ya kigaidi yaliyowahi kutokea nchini Kenya na kusababisha maafa
Kuna
taarifa kuwa watu ishirini wameuawa katika shambulio kwenye kijiji
Mashariki Kaskazini mwa Kenya. Mwandishi wa BBC anasema watu wenye
silaha walivamia kijiji cha Gunana katika County ya Wajir mapema siku ya
jumapili.
Amesema mapigano yalizuka kutoka na mgogoro baina ya koo mbili za Degodia na Gare. Ni mzozo wa mpaka baina ya koo hizo ambao wakuu wanautambua, lakini bado hawakuweza kuupatia ufumbuzi.
Aidha
mwandishi wa BBC ameongeza kuwa pamoja na kwamba kuliwahi kutokea
mapigano mengine hapo awali lakini hayajawahi kusababisha vifo vya watu
wengi kwa mara moja kama ilivyotokea siku ya jumapili.(P.T)
Mauaji
haya yanakuja wiki moja baada ya watu wapatao 60 kuuwawa katika
mashambulizi mawili yaliyotokea eneo la Mpeketoni katika pwani ya Kenya
lililodaiwa kufanywa na wapiganaji wa Al Shabaab .
Wapiganaji
hao walivamia vijiji viwili karibu na mji wa Mpeketoni, na kufanya
mashambulizi ambapo katika la kwanza lilisababisha mauaji ya wau 48 na
baadae la pili liliua watu wapatao 20.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment