VIKUNDI VYAKABIDHIWA MIZINGA NA MASHINE ZA KUKAMUA ASALI
Mgeni
rasmi Jesca Msambatavangu mwenye kashda ya Tanzania shingoni akiwa na
baadhi wa wavunaji wa asali kabla ya kwenda kuvuna asali na baadaye
katika hafla ya kukabidhiana mashine za kukamua asali na mizinga ya
nyuki pamoja na mavazi maalum ya uvunaji asali iliyofanyika katika
kijiji cha Kinywang’anga hivi karibuni.
Mgeni
rasmi Jesca Msambatavangu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Iringa akikabidhi kwa mmoja wa wenyeviti wa vikundi mashine ya kukamua
asali wakati wa hafla ya kukabidhiana mashine za kukamua asali na mizinga ya nyuki pamoja na mavazi maalum ya uvunaji asali. (J M)
Afisa Misitu mstaafu Teresphory Kahatano akitoa maelekezo kwa walinaji wa asali kabla ya kwenda katika mizinga ya nyuki.
MFUKO wa
Hifadhi ya Misitu Tanzania (TaFF) kwa kushirikiana na Mtandao wa Jamii
wa Usimamizi wa Misitu Kanda ya Kitapilimwa (MJUMIKK) umewakabidhi
mashine sita za kukamua asali na mizinga ishirini kwa vikundi vya
ujasiriamali vinavyojishughulisha na ulinaji wa asali katika kata za
Kitapilimwa na Kiwele katika jimbo la Ismani mkoani Iringa
Akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika kijiji cha
Kinywang’anga hivi karibuni, katibu wa mtandano wa MJUMIKK, Samson Fuko
alisema lengo la msaada huo ni kuleta ufanisi wa kulinda, kutunza na
kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza kipato cha
mwananchi mjasiriamali.
Alisema
mashine hizo zitakuwa shamba darasa la ufugaji wa nyuki na upandaji miti
utakaotumika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanachama wake na kutoa
elimu kwa jamii juu ya uhifadhi wa mazingira.
Fuko
alisema mtandao huo umefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama kutoka 50
waliokuwa mwanzao hadi wanachama 200 walioko sasa ambao unajihusisha na
ufugaji wa nyuki unaotekelezwa katika vijiji sita kati ya vijiji 11.
Alivitaja
vikundi vilifaidika na msaada huo kuwa ni Kinywang’anga, Faraja group,
Twiga group, Mshikamano. Jitegemee na kikundi cha Umoja vyote
vikipatiwa mizinga mashine na za kukamulia asali pamoja na mavazi
maalumu ya kuvaa wakati wa kulina asali vyote vikiwa na thamani ya sh.
milioni 4.5
Aidha
aliwataka wadau kuvisaidia vikundi vya ufugaji nyuki mizinga ya nyuki na
mbegu za miti kwa lengo la kuanzisha shamba darasa la ufugaji wa nyuki
na shamba darasa la upandaji miti na mavazi ya kuvunia asali kwa vikundi
hivyo.
Kwa
upande wake mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa
Jesca Msambatavangu aliyekuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya
mashine hizo amewaasa wazazi na walezi kuwahamasisha vijana kujiunga
katika shughuli za maendeleo wasiwaache wakilegalega kwani vijana hao
ndio nguvu kazi ya taifa
Alisema
maendeleo ya mtu hayaletwi kwa kukaa bila kujishughulisha na kukaa
vijiweni na kuwataka wajasiliamali hao kutumia fursa waliyoipata
kuitumia katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Aidha
Msambatavangu aliwahidi wafugaji nyuki kuwatafutia soko la bidhaa zao
kuweza kuwafikia watu wengi zaidi katika jamii ya mkoa wa Iringa na nje
ya nchi.
Msambataangu
ambae pia ni mlezi wa vikundi hvyo amewaeleza wananchi kuwa kiongozi
bora ni yule anaetekeleza majukumu aliyopewa na wananchi na sio
kuwadharau wale waliompa dhamana ya kuwa kiongozi
Msambatavangu
amewataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kuwatumikia na
kuwatatulia matatizo yao mda wowote wanapowahitaji na kuwajibika sio
kukaa na kutoa lawama.
Aidha
amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Pudensiana
Kisaka kwa kazi anayofanya ikiwa ni moja ya utekelezaji wa majukukumu
aliyopewa na serikali na amesema kuwa kiongozi huyo anapaswa kuigwa na
viongozi wa halimashauri nyingine kwani amekuwa akisikiliza matatizo ya
wananchi katika halimashauri yake na kuyafanyia kazi.
No comments:
Post a Comment