MAXIMO :KUJA YANGA ,APISHANA NA JUMA KASEJA
KOCHA
mpya wa Yanga, Marcio Maximo amezungumza moja kwa moja na Mwanaspoti
jijini hapa jana na akatamka maneno mazuri kwa mashabiki wa Yanga.
Mbrazil huyo amesema kwamba anakuja
Dar es Salaam kesho Jumatano(leo) kuitengeneza Yanga imara na
itakayobadili soka la Tanzania.
"Huu ndio
wakati muafaka kwangu kuifundisha Yanga, nataka niitengeneze Yanga kwa
masilahi ya nchi nzima, siendi Tanzania kwa ajili ya Yanga pekee naenda
kwa ajili ya Taifa, nataka kufanya kitu cha kipekee kabisa.
"Yanga ni
sehemu ambayo imetulia sana kwa sasa, nimekuwa nafuatilia sana. Najua.
Nimepata ofa za China, Dubai na klabu moja ya madaraja ya chini
Uingereza, lakini nimeamua kuziacha zote hizo niende Tanzania kwa
Yanga,"alisisitiza Maximo.
Kocha
huyo aliiambia Mwanaspoti jijini hapa kwamba kuna mambo machache
anamalizana na Yanga kisha atazungumza kwa kina zaidi kuhusiana na kila
kitu kupitia Mwanaspoti pekee.
Apishana na Kaseja
Wakati Maximo, akitua nchini kesho Jumanne, kipa wa timu hiyo Juma Kaseja yupo zake majuu anapiga dili.
Habari za
uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata kutoka wa mmoja wa marafiki wa kipa
huyo, zinasema Kaseja alitimka nchini wiki mbili zilizopita ambapo
alianzia Oman ambako aliongozana na Meneja wake Abdulfatah Saleh.
Baada ya
kutoka Oman sasa kipa huyo yupo Marekani ambapo kwa mujibu wa Abdulfatah
ambaye alizungumza na Mwanaspoti jana Jumapili, kipa huyo atakuwa huko
kwa wiki nzima na atarejea Jumapili wakati ambapo tayari Maximo atakuwa
ameshaanza kazi na wachezaji wengine wa Yanga kwenye Uwanja wa Bandari.
"Tupo Marekani mimi na Juma (Kaseja), kikubwa tumekuja kupumzika baada ya kumaliza majukumu yetu," alisema Abdulfatah
Yanga
wanakutana rasmi leo Jumatatu kwa matayarisho ya msimu mpya wa Ligi
lakini kabla ya mazoezi kutakuwa na kikao cha mabosi wa juu na mazoezi
yataanza rasmi kesho.
Ingawa
Ajenda za kikao hicho zikiwa siri Mwanaspoti linafahamu kuwa mambo
matatu yatazungumzwa ambayo ni nidhamu, mikakati mipya ya uongozi huo
pamoja na taarifa za ujio wa Maximo.
No comments:
Post a Comment