LIBYA:MSHUKIWA WA SHAMBULIZI MAHAKAMANI
Ahmed Abu Khatallah
Mmoja ya washukiwa
wakuu wa shambulizi lililomuua balozi wa Marekani nchini Libya miaka
miwili iliopita amefika mbele ya jaji katika mahakama moja ya kijimbo
mjini Washington, Marekani.
Ahmed Abu Khatallah alikana mashtaka yote matatu ya ugaidi dhidi yake.Mashtaka hayo yalisomwa kwake kupitia mkalimani.
Anashtakiwa kwa mauaji ya balozi Christopher Stevens pamoja na maafisa wengine watatu wa Marekani katika shambulizi la ubalozi wa Marekani mjini Benghazi.
Mshukiwa huyo alikamatwa na vikosi maalum na kusafrishwa kutoka Libya katika meli ya wanamaji wa Marekani.CHANZO BBC,(A.I).
No comments:
Post a Comment