Nigeria yakanusha maafisa wa jeshi wameshtakiwa
Maafisa
wa Nigeria wanakanusha ripoti kwamba maafisa wa jeshi 15 wakiwemo
majenerali 10 wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi kwa kushirikiana
na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.
Gazeti
moja nchini humo la The Leadership liliripoti kuwa maafisa hao walikutwa
na hatia ya kutoa taarifa na silaha kwa kundi la wanamgambo wenye
msimamo mkali ambalo linadaiwa kusababisha maelfu ya vifo katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita.
Jumatano,
maafisa wawili, msemaji wa jeshi, Meja Jenerali Chris Olukolade na
ofisa mawasiliano wa serikali Mike Olmeri wote waliiambia Sauti ya
Amerika-VOA kwamba taarifa hiyo sio ya kweli.
Serikali
ya Nigeria inapambana kuweza kulidhibiti kundi la Boko Haram licha ya
amri ya dharura iliyotangazwa huko kaskazini-mashariki na kupelekwa kwa
maelfu ya wanajeshi katika eneo. Kundi la Boko Haram limeshambulia
mashule, masoko, nyumba za ibada na vituo vya jeshi.(Martha Magessa)
Mashahidi
wanasema wanamgambo wakati mwingine wanavalia sare za kijeshi na mara
kwa mara wana nguvu zaidi kulioko wanajeshi. Kundi la Boko Haram bado
linawashikilia zaidi ya wasichana wa shule 200 waliowateka kutoka shule
moja katika jimbo la Borno, tukio lililotokea kati kati ya mwezi April.
CHANZO:VOA
No comments:
Post a Comment