TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, June 20, 2014

SUAREZ AIANGAMIZA ENGLAND KOMBE LA DUNIA

article-2662882-1EF0375200000578-441_634x329
MNYAMA` Luis Suarez akitokea katika majeruhi ya goti na kupangwa maalum kwa kuwaangamiza England ameweza kufunga mabao mawili Uruguay ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba watatu usiku huu.Suarez alifunga mabao yake katika dakika ya 39, lakini mshambuliaji wa England, Wayne Rooney akasawazisha bao hilo katika dakika ya 75 likiwa ni bao lake la kwanza katika fainali zote za kombe la dunia alizocheza.
Wakati England wakiamini watafunga bao la pili na kushinda mechi, alikuwa ni Suarez tena katika dakika ya 84 alipoachia shuti kali na kumuacha Joe Hart akiwa hana la kufanya na mpira kuzama nyavuni.
Kwa matokeo haya, England wamejiweka katika mazingira magumu kwasababu ni mechi ya pili wanapoteza.England inaweza kuwa timu ya kwanza katika fainali za kombe la dunia kupoteza mechi mbili za ufunguzi na kusonga mbele kama watafuzu hapa kwa kushinda magoli mengi na Costa Rica katika mchezo wa mwisho. (P.T)
Lakini hii inaonekana kuwa ndoto kwasabu hakuna uhakika wa England kuifunga Costa Rica kwa beki yao mbovu ambayo huwezi kuiamini hata dakika tano.Luis Suarez alifunga bao la pili kutokana na makosa ya beki ya England.
Mpira mrefu uliopigwa na mlinda mlango wa Uruguay Fernando Muslera, ulimpita kichwani nahodha Steven Gerrard, huku Gary Cahill akiwa amejisahau kabisa, na Suarez hakucheza na `nyani`, alifumua shuti na kuwaharibia usiku waingereza.
Dejected: England traipse off after the loss, knowing their World Cup is pretty much over
Wachezaji England wakiwa na huzuni baada ya kujua sasa michuano ya kombe la dunia inaweza kuwa bai bai.
In shock: Wayne Rooney looks like he cannot believe it after England's defeat by Uruguay 
Wayne Rooney anaonekena kama haamini kama England imepoteza mechi dhidi ya  Uruguay
Contrast: The ecstatic Uruguayans hug each other as a dejected Gary Cahill (right) is on his haunches
 Wachezaji wa Uruguay wakikumbatiana wakati Gary Cahill (kulia) akishangaa kilichowatokea.
Giving him a lift: Suarez is hoisted on to the shoulders of his team-mates after his match-winning display
 Lazima abebwe: Suarez akibebwa na wenzake baada ya kufunga mabao mawili
Match winner: Luis Suarez is ecstatic after scoring Uruguay's crucial second goal
 Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao la pili na la ushindi
Clinical: Suarez rifles the ball past Joe Hart in the England goal to win it for Uruguay
Suarez akifunga goli
Finally: Rooney runs off after scoring his first World Cup goal and England's equaliser
 Hatimaye amefunga: Rooney akishangilia goli lake la kwanza katika fainali za kombe la dunia tangua aanze kushiriki na la kusawazisha kwa England  usiku huu.
Coolly done: Rooney (right) slots the ball past Uruguay's goalkeeper Fernando Muslera to bring England level
Rooney (kulia) akimalizia krosi huku kipa wa Uruguay Fernando Muslera akijaribu kumzuia. 
Hapa chini ni vikosi vya timu zote mbili na viwango vyao. Alama ni juu ya 10. 
Kikosi cha Uruguay: Muslera 6, Gimenez 6, Godin 6, Caceres 6, Pereira 6; Lodeiro 7 (Stuani 67, 6), Gonzalez 6 (Fucile 78), Arevalo Rios 6, Rodriguez 6; Cavani 7, Suarez 8 (Coates 89). Subs: Munoz, Gargano, Hernandez, Forlan, Perez, Ramirez, Maxi Pereira, Silva.
Kadi ya njano: Godin.
Mfungaji: Suarez 39, 84.Kikosi cha England: Hart 6, Johnson 5.5, Cahill 6, Jagielka 5, Baines 5.5; Gerrard 5.5, Henderson (Lambert 87) 6; Sterling 5 (Barkley 64, 6), Rooney 6, Welbeck 4.5 (Lallana 71, 6), Sturridge 6.5. Subs: Foster, Wilshere, Lampard, Smalling, Jones, Milner, Shaw, Forster.
Kocha: Roy Hodgson 6.5
Kadi ya njano: Johnson.
Mfungaji: Rooney 75.Mchezaji bora wa mechi: Luis Suarez.
Mwamuzi: Carlos Velasco Carballo (Spain).
Chanzo:Shaffihdauda.com

No comments:

Post a Comment