BRAZUKA: Yanayojiri nchini Brazil siku mbili kabla ya Kombe la dunia kuanza
Zikiwa
zimebakia takribani siku mbili kabla ya michuano ya kombe la dunia
ambayo ni mikubwa kabisa kwa upande wa soka ikiwa inayovutia mabilioni
ya watazamaji duniani kuanza
Mtu mmoja amefariki na
wengine kujeruhiwa baada ya sehemu iliyokuwa ikijengwa kuporomoka,
katika harakati za kumalizia ujenzi muhimu wa eneo linaloitwa Monorail,
taarifa kutoka Sao Paulo zimesema.
Ni eneo la kilomita 17 lililokuwa litumike kuunganisha uwanja wa ndege na mfumo wa usafiri wa reli mjini humo.Brazil imekuwa ikisuasua na sasa inaharakisha kumalizia majengo na miundo mbinu iliyopangiwa kutumika wakati wa kombe la dunia.
Visa vya ajali kuhusiana na ujenzi huo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.
Wafanyikazi wanane walifariki wakati wa ujenzi wa eneo la katika la uwanja wa kombe la dunia ‘arena’.
Wakati huo huo migomo inayoendelea nchini imetengeneza tena headlines.
Mgomo wa
wafanyakazi wa usafiri mjini Sao Paulo, Brazil umehairishwa kwa siku
mbili, kwa ajili ya kupisha mazungumzo baina ya serikali na wafanyakazi.
Hata hivyo wafanyakazi wametishia kugoma tena alhamisi siku ya
ufunguzi wa kombe la dunia iwapo wenzao 60 wanaokabiliwa na tisho la
kufutwa kazi hawatarudishwa kazini.Serikali haijaafiki nyongeza ya 12% wanayodai wafanyakazi hao, wala kuwarudisha kazini wafanyakazi waliosimamishwa.
Nyongeza ya asilimia 8.8% waliokubali kutoa serikali imekataliwa na wafanyakazi hao.
Mfumo huo wa usafiri wa reli ya mjini uitwao ‘Metro’ umekumbwa na mgomo wa tangu alhamisi iliyopita.
Kinyume na matarajio kombe hilo la dunia limewagawanya raia wa nchi hiyo kiasi cha kuushangaza ulimwengu unaoitambua Brazil kama gwiji wa soka.
Kuna wale wanaoghadhabishwa kwamba migomo hiyo inaharibu si tu sifa hizo za Brazil bali pia kuwaongezea kero la foleni na msongamano unaovuruga ratiba zao mijini, lakini wengine wamechukulia fursa hiyo ya kombe la dunia kutetetea maslahi yao kama kudai nyongeza ya mishahara na huduma nyenginezo za kijamii kutoka kwa serikali.
Rais wa nchi hiyo Bi Dilma Rousseff amesema kamwe hataruhusu maandamano ya ghasia kuvuruga michuano hiyo ya kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment