MWANAMKE ALIYEASI DINI SUDANI AACHIWA HURU
Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini ameachiliwa huru.
Wakili wake ameambia BBC kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu
Hukumu
ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama
ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.
Meriam
ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya
kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukata kukana kuwa yeye ni
mkristo.
Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment