TALEBAN LAWAKATA VIDOLE WALIOPIGA KULA
Raia waliopiga kura nchini Afghanistan wakatwa vidole
Maafisa
nchini Afghanistan wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi
mmoja wa uchaguzi baada ya gari lao kazkazini mwa taifa hilo kukanyaga
bomu lililotegwa barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa
urais wa raundi ya pili.
Katika tukio jengine kundi la Taleban liliwakata vidole baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.
Zaidi ya watu 60 wameuawa na wanamgambo hao katika misururu ya mashambulizi wakati wa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.
Raia wa
taifa hilo wanachagua kati ya aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni
Abdulla Abdulla na Ashraf Ghani ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa
fedha.
Wagombea wote wameahidi kuimarisha uhusiano na mataifa ya magharibi mbali na kukabiliana na ufisadi.(P.T)
No comments:
Post a Comment