WASUNNI WATEKA ANBAR,MAGHARIBI MWA IRAQ

Wapiganaji wa Isis wakifanya gwaride
Wanamgambo
 wa Kisuni nchini Iraq wamechukuwa uthibiti kamili wa mipaka yote ya 
taifa hilo na mataifa ya Syria na Jordan baada ya kuteka maeneo mawili 
ya mwisho ya vivuko vya mpakani katika mkoa wa magharibi wa Anbar nchini
 Iraq.
Maafisa 
wa usalama wamesema kuwa waasi hao wanaoongozwa na kundi la wanamgambo 
wa madhehebu ya kiislamu wa Kisunni maarufu kama ISIS wameteka eneo la 
al-Waleed lililopo karibu na mpaka wa Syria na mji wa Turaibil uliopo 
njiani kuelekea nchini Jordan.
Mapema Jumapili wanamgambo hao waliteka miji mingine mitatu Magharibi mwa nchi hiyo.(P.T)
        
Serikali 
ilisema kuwa katika maeneo fulani, wanajeshi wameondoka kimpango. 
Mwanachama Msuni maarufu nchini, Shaikh Raad al-Suleiman, kutoka Ramadi,
 alisema kuwa ni idadi ndogo tu ya wanachama wa ISIS wameingia katika 
Mkoa wa Anbar.
"Ndio 
kuna wanachama wachache wa Isis ambao wameingia katika Mkoa wa Anbar, 
wachache sana, hawazidi asilimia tano, lakini inaonekana wanachama wa Al
 Qaida na wakaazi wa vijiji hivyo wenye itikadi kali wanashirikiana. 
Ushirikiano unaotakana na haja ya wanavijiji kutaka kujilinda," 
al-Suleiman alisema.
Awali 
katika mahojiano kwenye kipindi cha televisheni cha CBS Face the Nation,
 Rais Obama alieleza hatari inayoweza kuletwa na kundi la wapiganaji la 
ISIS. Alisema kundi hilo ni hatari ya muda mrefu kwa Marekani na huenda 
kundi hilo likatenganisha wakaazi wa maeneo yote waliyoteka kutoka kwa 
maeneo mengine ya dunia.
"Msimamo 
wao mkali unatishia usalama wa sasa na wa muda mrefu ujao. Kuna makundi 
mengine kule nje ambayo pengine yana mipango hatari zaidi ya wakati huu 
inayolenga Marekani ambayo lazima sisi kama Marekani tujitahadhari nayo
Ukweli wa
 kundi kama hili ni kuwa kwa kawaida linapoteka eneo fulani, kwa sababu 
wao huwa wakatili, kwa sababu wana misamamo mikali, baada ya muda fulani
 wakaazi wa maeneo hayo huwakataa. Tushawahi kushuhudia hayo mara kwa 
mara. Tulishuhudia hayo katika Vita vya Iraq katika maneo kama vile Mkoa
 wa Anbar ambako makabila ya Kisuni yalibadilima mara moja na kuazi kwa 
sababu ya mwongozo wa itikadi kali," Rais Obama alisema.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment