ISIS YACHAPISHA PICHA ZA MAUAJI IRAQ
Vuguvugu la Sunni
lenye msimamo mkali la ISIS ambalo limeteka maeneo ya Kaskazini mwa Iraq
limesambaza picha ambazo zinaonyesha jinsi wapiganaji wake
walivyoangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa Iraq.
Picha zinazosambazwa kupitia internet
zinaonyesha miili ya watu iliyosongamana ndani ya mtaro ikiwa imepelekwa
hapo kwa kutumia malori.Wapiganaji wa ISIS wanaonekana wakibeba bendera nyeusi ya huku wakichoma miili hiyo na kulazimisha mateka kulala chini.
Msemaji wa jeshi nchini mjini Baghdad amesema anaamini kuwa picha hizo ni halali.
BBC haijaweza kuthibitisha uhalali ya picha hizo kikamilifu lakini iwapo ni za kweli mauaji hayo yatakuwa mojawapo ya matukio mabaya zaidi kuwahi kuikumba Iraq tangu majeshi ya Marekani kuingia nchini humo mwaka 2003.
Awali video iliyorekodiwa ilionyesha mamia ya watu wakilazimishwa kuelekea katika kityuo kimoja huku sauti ikieleza kuwa ni wanajeshi waliokubali kushindwa.
Duru kutoka vuguvugu la waasi zinasema idadi kubwa ya watu waliotekwa wameuawa.
Mji wa Tikrit ulitekwa na waasi Jumatano wiki iliyopita na majeshi ya Iraq yalikubali kushindwa bila pingamizi.CHANZO BBC,(A.I).
No comments:
Post a Comment