IRAQ YAOMBA MSAADA WA KIJESHI KWA MAREKANI

Mkuu wa 
majeshi ya Marekani anasema Iraq imeiomba Marekani kusaidia kufanya 
mashambulizi ya anga ili kupambana na wanamgambo wa ki-Islam wa ki- 
sunni ambao wamechukua udhibiti wa miji muhimu ya kaskazini na 
wanaitishia kuishambulia Baghdad.
        
Mwenyekiti
 wa baraza la wakuu wa majeshi, Jenerali Martin Dempesy, ali-iambia 
kamati ndogo ya baraza la seneti la Marekani hapo jumatano kwamba 
serikali ya Iraq imeshindwa kuwalinda wananchi wake na amesikitishwa 
sana na jambo hilo.
Naye 
waziri wa ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel alisema viongozi wa kishia 
nchini Iraq, hawajawahi kutekeleza jukumu lao la kuunda serikali ya 
umoja wa kitaifa pamoja na wasunni na wakurdi.
Wakati 
huo huo, akisafiri kuelekea Colombia, Makamu Rais wa Marekani, Joe Biden
 alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki 
pamoja na viongozi wa kisuni na wa kikurdi. Alisisitiza juu ya umuhimu 
wa serikali ya umoja nchini Iraq ambayo itaweza kukabiliana na kitisho 
kinachosababishwa na wanamgambo, kwa wa-Iraq wote
CHANZO BBC
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment