OBAMA AOMBA PESA AWASAIDIE WAASI

Rais Barack Obama wa Marekani
Rais wa 
Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola 
milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha 
Waasi wa Syria.
Bado 
haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekani itautoa 
japo kulikuwa na maombi ya waasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya
 kubeba ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha
 hizo zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ikiwa 
Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama,hii itakuwa mara ya kwanza kwa 
Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria, 
mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini
 Syria.
Waasi wa 
Syria wanapambana na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa ISIS, ambalo
 ni kundi la waislamu ambao pia wameteka mpaka ndani ya nchi ya Iraq.(P.T)
No comments:
Post a Comment