Vikosi vya Iraq vyashindwa kuteka Tiqrit
mwanajeshi wa Isis
Ripoti
kutoka Iraq zinaarifu kuwa vikosi vya serikali vilivyojaribu kuuteka mji
wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa kisunni vimelazimika kurejea nyuma.
Walioshuhudia
wanasema kuwa wanajeshi hao walilazimika kurudi katika mji wa Dijla
,yapata kilomita 25 kusini baada ya mashambulizi yao yalioshirikisha
mizinga,magari ya kujihami na ndege kushindwa kufua dafu.
Hatahivyo kuna ripoti ya majeruhi wengi kutoka pande zote mbili.
Duru
zimearifu kuwa vikosi hivyo vya serikali vinajitahidi kufika Tikrit kwa
kuwa wapiganaji wa ISIS wametega vilipuzi vingi katika barabara kuu ya
kuingia mjini humo.
Wakati
huohuo Iraq inasema kuwa imepokea kundi la kwanza la ndege za kijeshi
ilizoagiza kutoka Urusi ili kuisadia kukabiiana na wapiganaji wa dhehenu
la kisunni ISIS ambao wameyateka maeneo mengi ya taifa hilo.BBC,(A.I).
No comments:
Post a Comment