Yusuf Manji aingilia uchaguzi Simba
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, ametoa ya moyoni kuhusiana na mchakato wa uchaguzi wa Simba.
Mfanyabiashara
huyo ametoa angalizo kwamba Simba inapaswa kufanya hatua za makusudi
kupata viongozi imara na kuachana na malumbano ambayo hayajengi.
Uchaguzi
wa Simba umekumbwa na hali ya sintofahamu baada ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kutangaza kuusitisha kabla ya Mwenyekiti wa klabu hiyo,
Ismail Aden Rage na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Damas Ndumbaro
kuibuka na kusema TFF haina mamlaka hayo.(P.T)
Awali
kulikuwa na taarifa kuwa baadhi ya viongozi na wapenzi wa Yanga
walifurahishwa na taarifa za kurejeshwa kwa mgombea urais, Michael
Wambura katika mchakato wa uchaguzi kwa madai kuwa wanakubaliana na
misimamo yake.
Akizungumza
na Mwanaspoti ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Manji alisema Simba
na Yanga zinategemeana na endapo timu moja kati ya hizo itakwama ni
dhahiri kuwa madhara yake yatauathiri upande wa pili, hivyo asingependa
kuiona klabu hiyo ikiingia kwenye vurugu na kushindwa kufanya uchaguzi
wake kwa amani.
"Maendeleo
ya soka la nchi hii yanategemea Simba na Yanga, hizi ni kama mapacha
kwani moja ikiporomoka nyingine nayo inaonja chungu ya jiwe kwani
haiwezi kuwa na msisimko kama uliokuwa mwanzo, natamani kuona Simba
ikifanya uchaguzi wake kwa amani na kupata viongozi imara," alisema
Manji.
"Kukiwa
na utulivu katika klabu hizi mbili ni dhahiri kuwa tunaweza kuujenga
mchezo wa soka nchini, klabu hizi zitasaidia kuijenga Taifa Stars hivyo
nisingependa kuona moja inapoteza mwelekeo."
Mbali ya
uchaguzi huo, Mwenyekiti huyo ameitaka TFF kuzungumza na na wadhamini wa
klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuwaongezea fedha za udhamini
kwani kampuni hiyo inatoa fedha nyingi zaidi kwenye timu ya taifa,
Taifa Stars wakati klabu ndiyo ngazi ya wachezaji kupanda kuchezea
Stars.
"Nashangaa
kuona TBL inatoa fedha nyingi zaidi Stars kuliko sisi (Yanga) na Simba,
tunaotoa wachezaji kwenda kucheza timu hiyo ya taifa , nawaomba
walifikirie hilo mara mbili," alisema Manji.
Chanzo:Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment