TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, June 17, 2014

Ujerumani 4-0 Ureno

140616173322_wc2014germany_thomas_mueller_512x288_ap_nocredit_042ff.jpg
Thomas Mueller ndiye mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja Brazil
140616164445_pepe_512x288_getty_nocredit_dff56.jpg
Pepe alionesha kadi nyekundu baada ya kumgonga kichwa Mueller
Thomas Muller alifunga mabao matatu na kuisaidia Ujerumani kuishinda Ureno mabao
manne kwa nunge.
Mlinzi wa Ureno, Pepe alionyeshwa kadi nyekundu na kuondolewa katika mchuano huo.
Ujerumani, mabingwa mara tatu wa kombe la dunia, walionyesha mchezo wa kiwango cha juu.
Ujerumani ilichukua uongozi pale ambapo Thomas Muller alipopiga mkwaju wa penalti, baada ya Joao Pereira kuchezea vibaya Mario Goetze.
Mart Hummels alifunga bao la pili kupitia kichwa.
Pepe alionyeshwa kadi nyekundu muda mfupi baadaye kwa kosa la kumgonga Muller kwa kichwa.
Muller alifunga bao la tatu, ambalo lilikua lake la pili katika mchuano huo, kwa mkwaju wa kutoka karibu na lango.
Katika dakika ya 77, Thomas Muller aliongeza bao la nne la Ujerumani na kufanya idadi ya mabao yake katika mchuano huo kuwa matatu.
Muller anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja, kwenye kombe hili la dunia, mwaka 2014.
Kufuatia ushindi huu, Ujerumani inaongoza kundi hili kwa alama tatu.CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment