ISRAEL YASEMA HAMAS ILIWAUWA VIJANA WAKE
Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa miili hiyo ilikuwa chini ya miamba iliopo kwenye mji wa west Bank wa Hebron.

Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu
Israel imepeleka vikosi vyake katika kijiji cha Palestina cha Hal-hul.
Katika
 kikao cha dharura cha mawaziri ,waziri mkuu wa Israel Benjamin 
Netanyahu amesema vijana hao walitekwa na kuuawa katika mauji aliyosema 
yamefanywa na wanyama.
Netanyahu amelilaumu kundi la Wapalestina la Hamas, na akaahidi kulipiza kisasi.
Hamas imekana kuhusika na mauaji hayo kupitia mshauri rasmi wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas -Abdallah Abdallah
Mwandishi
 wa BBC aliyeko mashariki ya kati anasema milio ya mashambulizi ya ndege
 za Israeli imesikika kote katika ukanda wa Gaza .
Kulikuwa na tetesi kuwa Israeli ingeileng maeneo ya Hamas baada ya kikao chake cha mawaziri cha usalama .
Mji
 wa Gaza umesalia kuwa ngome kuu ya Hamas na ofisi zake katika eneo hilo
 zimekuwa zikivamiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili na nusu.
vifo vya karibu wapalestina watano vimeripotiwa na mamia ya wapalestina wamekamatwa.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment