MAREKANI YAANZA KUISAIDIA IRAQ VITANI

Wanajeshi wa Marekani
Wizara ya
 Ulinzi nchini Marekani imesema kuwa kundi la kwanza la wanajeshi wa 
Marekani waliotumwa kulisaidia jeshi la Iraq kupambana na machafuko ya 
waasi wa kisunni limeanza kazi.
Rais 
Obama alitangaza juma lililopita kuwa wanajeshi maalum 300, walitumwa 
Baghdad kuwapa mawaidha na kuwasaidia maafisa wa huduma za usalama, na 
kuwa takriban nusu ya idadi ya wanajeshi hao tayari imewasili Baghdad 
katika shughli hizo, na waliosalia wanatarajiwa kuwasili siku chache 
zijazo.
Wanajeshi 40 wa Marekani walio nchini Iraq ndio kikosi cha kwanza kilichotumwa nchini humo.(P.T)
        
Katika siku chache zijazo, wanajeshi wengine kutoka sehemu nyingine za eneo hilo watakua wakiwasili Baghdad.
Utawala 
wa Obama umekua na kibarua kigumu kueleza kuwa wanajeshi hao hawakua na 
nia ya kutumika kivita ila lengo lao haswa ni kutoa ujasusi kuhusu hali 
ilivyo nchini humo.
Serikali ya Iraq ilikuwa imeitisha msaada wa mashambulizi ya angani ya Marekani ili kujaribu kuzuia hatari ya ISIS.
Hata 
hivyo, rais Obama amesita kufanya chochote kitakacho sababisha shutma za
 Marekani kuegemea upande mmoja, katika mgongano huo wa kidini.
Mara kwa 
mara imekua akiitisha suluhisho la kisiasa kwa mgogoro huo, kupitia kwa 
serikali inayowasilisha vizuri matakwa ya wa Sunni na waKurdi walio 
wachache.
Hili lisisitizwa siku ya Jumanne na waziri wa mswala ya kigeni wa Marekani, John Kerry, alipoutembelea mji la kikurdi wa Irbl.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment