TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, June 10, 2014

Wanawake wengine 20 watekwa Nigeria

boko
Watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la Boko Haram wamewateka takribani wanawake 20 karibu na eneo walikowateka wasichana 200 wa shule Kaskazini mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanawake hao waliingizwa ndani ya magari wakiwa wamenyooshewa mitutu ya bunduki na kupelekwa katika eneo lisilojulikana katika Jimbo la Borno.
Jeshi la Nigeria ambalo limekuwa likikosolewa kwa kushindwa kuzuia vitendo vya kigaidi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo bado halijasema chochote kuhusiana na tukio hilo.
Licha ya hali ya tahadhari iliyotangazwa katika ukanda huo wakazi wa eneo hilo wanasema jeshi limekuwa halifanyi chochote au wakati mwingine kutokuwepo kabisa katika eneo hilo na kuruhusu kundi la Boko Haram kuendelea kufanya mashambulizi yake.
Kidnapped schoolgirls are seen at an unknown location in this still image taken from an undated video released by Boko Haram
Kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi kadhaa tangu mwaka 2009 kushinikiza kuanzisha Jimbo litakalofuata sheria za kiislamu nchini Nigeria ambapo hadi sasa maelfu ya watu wameuwawa katika mashambulizi hayo.
Tukio la hivi karibuni zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa katika kijiji cha Chibok karibu na mpaka wa Cameroon April 14 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment