TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, June 13, 2014

NEYMAR AING’ARISHA BRAZIL KOMBE LA DUNIA, YAICHAPA CROATIA 3-1


 Neymar amefunga mabao mawili Brazil ikishinda 3-1 dhidi ya Croatia usiku huu
Spot on (just about): Neymar puts his penalty past Stipe Pletikosa despite the Croatia keeper getting a hand to it
Neymar akimfunga kwa penalty kipa Stipe Pletikosa wa Croatia aliyekaribia kuokoa mkwaju huo kama si kuupangulia nyavuni kwake(P.T)
Na Nurat Mahmoud, SAO PAULO
MWANZO mzuri kwa Neymar akifunga mabao mawili usiku huu, wenyeji Brazil wakianza vyema Fainali za Kombe ka Dunia kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Croatia Uwanja wa Corinthias, mjini Sao Paulo.
Croatia waliotawala sehemu ya kiungo, waliuanza vizuri mchezo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 11.
Sifa zimuendee Olic aliyepiga krosi nzuri kwa Nikica Jelavic na katika harakati za kuokoa, Marcelo wa Brazil aliutumbukiza mpira kwenye lango lake.
Croatia waliendelea kutawala mchezo baada ya bao hilo, lakini Brazil waiendelea nao kupambana kusaka bao la kusawazisha.
Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 29 baada ya Neymar kuisawazishia Brazil kufuatia shambulizi la kushitukiza- baada ya kipa Julio Cesar kuokoa mpira wa kichwa wa Jelavic na kuanzisha shambulizi haraka.
Brazil ilipata bao la ushindi kwa penalti dakika ya 71 baada ya Fred kujiangusha wakati anakabiliana na Dejan Lovren kwenye eneo la hatari na Neymar akaenda kufunga tena.
Oscar alihitimisha ushindi wa Brazil kwa bao la tatu dakika ya 90 na ushei na kuwapa faraja mashabiki wa nyumbani.
Kikosi cha Brazil kilikuwa: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Paulinho/Hernanes dk63, Gustavo, Hulk/Bernard dk68, Oscar, Neymar/Ramires dk88 na Fred.
Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Lovren, Vrsaljko, Modric, Rakitic, Perisic, Kovacic/Brozovic dk61, Olic na Jelavic/Rebic dk78.

No comments:

Post a Comment