MBUNGE DODOMA KUNG'ATUKA
MBUNGE wa
Chilonwa, Hezekiah Chibulunje (CCM), ametangaza kutogombea tena ubunge
wa jimbo hilo mwakani baada ya kulitumikia kwa miaka 20 mfululizo.
Chibulunje
alisema jana kuwa anastaafu ubunge ili kupisha vijana nao waongoze
jimbo hilo alilosema limepiga hatua kubwa kimaendeleo.
Alisema
amekuwa mbunge kwa vipindi vinne mfululizo na kwamba katika miaka hiyo
20, miaka kumi alikuwa Naibu Waziri ikiwemo katika Wizara ya Ushirika na
Masoko mwaka 2000 hadi 2005.
Alibainisha
kuwa, kuanzia mwaka 2006 hadi 2010, alikuwa Naibu Waziri katika wizara
kadhaa alizozitaja kuwa ni Kilimo, Chakula na Ushirika; Viwanda na
Biashara; Kazi; na Miundombinu.
“Katika
nafasi zote hizi, za ubunge na unaibu waziri, sijawahi kupata
misukosuko,” alisema Chibulunje na kutaja mafanikio katika jimbo hilo
kuwa kupitika kwa barabara zote zikiwemo za tarafa ya Itiso, tofauti na
alipoingia madarakani mwaka 1995
Pia,
alisema kwa sasa asilimia 86 ya wakazi wa jimbo lake wanapata majisafi
na kwamba, vijiji vitatu tu ambavyo vina shida ya maji, ambavyo ni
Mlimwa kata ya Membe, Azimio kata ya Manyemba na Majengo kata ya
Chiwondo.
Kwa
upande wa umeme, alisema asilimia 90 ya vijiji vya jimbo hilo, vitakuwa
na umeme ifikapo mwakani. Umeme huo unasambazwa na Wakala wa Umeme
Vijijini (REA).
Kuhusu
elimu ya sekondari, Chibulunje alisema alisema alipoingia madarakani
mwaka 1995, jimbo hilo lilikuwa na sekondari moja ya Chamwino, lakini
sasa kata zote 13 zina sekondari.
CHANZO:HABARILEO
No comments:
Post a Comment