CFAO YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WAMILIKI WA MALORI YA MERCEDES BENZ NCHINI
Msimamizi
wa ufundi wa Magari aina ya Mercedes Benz kutoka kampuni ya CFAO Motors
Bw. Winner Mushi (wa tatu kushoto) akionyesha matumizi ya kifaa maalum
cha ukaguzi wa Malori ya Mercedes Benz (Star Diagnosis Machine) kwa
baadhi ya mafundi na wasimamizi wa ufundi wa magari ya kampuni ya
Bakhresa Group.
Bakhresa
Group ni mmoja wapo wa wateja wa CFAO Motors ambao wanamiliki malori ya
Mercedes Benz. Bw. Heico Herzog Mtaalamu wa ufundi (Flying Doctor)
kutoka Mercedes Benz Ujerumani,(wa tatu kulia) akisimamia shughuli hiyo
iliyoendeshwa na Bw. Mushi.
Wengine
ni Key Account Manager wa Mercedes Benz, Bw. George Washington (kulia),
Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah
Seif (kushoto), Jarangi Nyabagara ambaye ni fundi wa Mercedes Benz (wa
pili kushoto), na aliyechuchumaa ni Mohammed Shariff Meneja wa Karakana
ya Bakhresa Group.
Na Mwandishi Wetu,
KAMPUNI
ya CFAO Motor Tanzania hivi karibuni imezindua huduma mpya ya “Service
Camp” ambapo chini ya huduma hii wa wamiliki wa malori yanayotengenezwa
na Mercedez Benz watapata huduma ya ukaguzi bure na mafunzo kwa madereva
wao.
Akizungumza
na mwandishi wetu, jijini Dar es Salaam Key Account Manager wa Mercedez
Benz, Bw George Washington amesema kwamba wameamua kuanzisha huduma
hiyo ili kuweza kuwahudumia wamilimi wa magari hayo kwa karibu zaidi.
“Mpango
huu utapeleka huduma karibu na wateja na kwa kuwa hapo mwanzo wamiliki
wa malori walikuwa hawapati huduma za matengenezo vizuri barani Afrika,”
amesema
Amesema
kuwa kuna upungufu katika kuwahudumia wamiliki wa malori ya Mercedez
Benz Afrika na hivyo wameona ni busara kuja na ‘Service Camp’ ili
kuwapeleka wateja huduma za matengenezo na mafunzo kwa madereva wao huko
walipo.
Aliongeza
kwamba huduma hiyo ya ‘Service Camp’ itakuwa ikitolewa kwa njia mbili
tofauti ambazo ni kwenda kwa mteja na kukagua malori bila gharama
yoyote.
Amesema
kwamba vile vile chini ya huduma hiyo watakuwa wakitoa mafunzo kwa
madereva wa malori ili waweze kujajua vizuri magari hayo pindi
wanapopata tatizo la kiufundi.
Bw.Washighton
aliongeza kwamba vile vile watakuwa wanawafundisha madereva jinsi
vipuri vya Mercedez Benz vinavyopaswa kuwa ili kuweza kutambua vipuri
bandia kwenye soko la nchini au karakana mbalimbali.
“Tunawaonesha
vipuri halisi na vipuri bandia kwa sababu kuna madhara katika kutumia
vipuri bandia ambapo madhara yanaweza yasionekane katika muda wa siku
chache bali huonekana baada ya muda mrefu,”
“Ukianza
kuangalia gharama ya kutengeneza gari baada ya madhara kutokea unakuta
gharama yake ni kubwa kuliko ambapo ungetumia vipuri halisi,” alieleza
Bw Washington.
Alisisitiza
kwamba kwamba hatua ya pili ni kuweka kambi barabarani ambapo malori
mengi ya Mercedes Benz yanapita, hivyo kila ambaye anamiliki lori aina
ya Mercedes Benz na anataka kufanyiwa ukaguzi, hupata huduma hiyo bila
gharama, na hatimaye taarifa kamili zake za ukaguzi kurudishwa kwa
mmiliki wake.
Washington
amesema kwamba kampuni ya CFAO inataka kuwa karibu zaidi na wateja
wake, kwani inataka wateja waone kwamba kuna watu wanaowajali ili
kudumisha na kuimarisha uhusiano kati yao na wateja wao.
Muuzaji
wa vipuli vya magari ya Mercedes Benz nchini kutoka kampuni ya CFAO
Motors, Emmanuel Sembua akimfafanulia jambo Meneja wa Usafirishaji
kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif jinsi ya kutambua
vifaa feki vya magari vya Mercedes Benz ili kujieupusha na matapeli ya
vifaa hivyo.
“Tunataka
wateja wetu waone kwamba iwapo magari yao yanapata matatizo, kuna watu
ambao watawafuata na kuwahudumia kwa wakati unaofaa. Kama unavyojua haya
ni malori kwa ajili ya transport business, hivyo hayapaswi kuwa mabovu
kwa wakati mrefu kwa kuwa hiyo itawasababishia hasara wateja wetu.
Wameyanunua ili wayatumie kwenye biashara na kazi zao, sasa, yakiwa out
of service, hiyo ni hasara, na sisi hatutaki wateja wetu wapate hasara,”
aliongeza Washington.
Alipoulizwa
kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo ya “Service Camp”, Washington amesema
kwamba hii ni mara ya kwanza huduma hiyo kupatikana hapa nchini, ila
kwa nchi jirani ya Kenya, huduma hiyo imeshapatikana mara tatu.
Aliongeza kwamba huduma ya “Service Camp” itapatikana tena mwezi Novemba
mwaka huu.
“Tutaitoa
huduma hii kwa muda mfupi hapa Dar es Salaam kisha tutahamia mikoani na
huu ni mpango endelevu, sio kitu cha mara moja,” alisisitiza.
Akizungumzia
kuhusu huduma iliyotolewa kabla ya kuanzishwa kwa “Service Camp”,
Washington amesema kwamba awali walikuwa na huduma inayoitwa “Technical
Exchange”, ambayo ilikuwa na lengo ya kubadilishana uzoefu wa kiufundi
kati ya wasimamizi wa karakana za wamiliki wa magari hayo na mafundi wa
CFAO.
Meneja
wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif na
Meneja wa Karakana ya Bakhresa Group, Mohammed Shariff wakipewa maelezo
na Muuzaji wa vipuli vya magari ya Mercedes Benz nchini kutoka kampuni
ya CFAO Motors, Emmanuel Sembua (kulia) ya Battery zinazouzwa na kampuni
ya CFAO Motors yenye garantii na uwezo mkubwa kwa malori.
“Tumegundua
kwamba baada ya kuifanya hii technical exchange kumekuwa na mafanikio
makubwa sana na tumeenda mbele na kuiboresha zaidi na tutafika wakati
ambapo kutakuwa na washindi, kwani tumeona tuwashindanishe hawa mafundi
wakuu kwa nia ya kuongeza ufanisi wao ili waweze kuyasimamia magari ya
waajiri wao vizuri zaidi.
“Kutakuwa
na washindi ambao tutawapeleka Ujerumani, kule kwenye kiwanda, ili
waweze kuona jinsi ambavyo magari yanaundwa na kusimamiwa,
“kuanzia
ubunifu hadi majaribio na mwisho kwenda kiwandani kwa ajili ya uundwaji.
Huu ndio mpango ambao tunao hivi sasa na mpaka mwaka kesho tutakuwa
tumempata mshindi ambaye tutampeleka Ujerumani ili atuwakilishe kule na
kuona jinsi mambo yanavyoendesha. Kwa mantiki hii mpango huu nao pia ni
mpango endelevu,” amesema Washington.
Washington
alihitimisha na kusema kwamba mpango huu wa “Service Camp” unahusu
magari ambayo ni malori pekee yaani Atos, Actros na Atego, na kwamba
magari madogo hayatahusishwa na mpango huu.
Picha ya pamoja baada ya zoezi hilo.
Amesema
kwamba kwa sasa huduma hii inapatikana kwenye karakana zilizopo kwenye
ofisi za CFAO zilizopo Barabara ya Nyerere na kwa upande wa Road
Inspection, wamiliki wa malori ya Mercedes Benz watajulishwa mapema.
Aliongeza
kwamba kuhusu mwezi Novemba, kituo kikuu cha kwanza nje ya Dar es
Salaam kitakuwa Kibaha kwa kuwa barabara hiyo inatumiwa na magari mengi
yanayokwenda mikoani.
Hatimaye, vituo vingine ambavyo vimepangwa vitatangazwa mapema iwezekanavyo ili wateja wa CFAO wapate muda wa kutosha kujiandaa.
No comments:
Post a Comment